This site uses cookies in order to function as expected. By continuing, you are agreeing to our cookie policy.
Agree and close

News Tangazo la Kujiunga na Mafunzo ya Stashahada na Astashahada Mwaka wa masomo 2015/2016

Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA-LIVESTOCK TRAINING AGENCY) inatangaza nafasi za mafunzo katika ngazi ya Astashahada na Stashahada kwa mwaka 2015/2016.

Concerned URL http://www.mifugouvuvi.go.tz
Source LIVESTOCK TRAINING AGENCY
Release date 10/07/2015
Geographical coverage DAR ES SALAAM,
Keywords Mafunzo, LITA,

TANGAZO LA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA STASHAHADA NA ASTASHAHADA KATIKA WAKALA WA VYUO VYA MAFUNZO YA MIFUGO (LIVESTOCK TRAINING AGENCY) KATIKA MWAKA WA MASOMO 2015/16


1. Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA) inatangaza nafasi za mafunzo katika ngazi ya Astashahada na Stashahada kama ifuatavyo:

 • Stashahada ya Afya na Uzalishaji wa Mifugo (Diploma in Animal Health and Production - DAHP)
 •  Astashahada ya Afya na Uzalishaji Mifugo (Animal Health and Production Certificate - CAHP)
 •  Astashahada ya Ufundi Sanifu wa Maabara (Certificate in Veterinary Laboratory Technology - CVLT)
 •  Stashahada ya Ufundi Sanifu wa Maabara (Diploma in Veterinary Laboratory Technology
 • (DVLT)
 •  Stashada ya Uendelezaji wa Nyanda za Malisho na Udhibiti wa Ndorobo (Diploma in Range Management and Tsetse Control)

2. Stashahada Maalum ya Teknolojia ya Maziwa (Speciliased Diploma In Dairy Technology) Katika mwaka wa fedha wa 2015/2016, Serikali kupitia Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA) itatoa mafunzo kwenye Kampasi zake sita na vituo vyake viwili; Tengeru, Mpwapwa, Morogoro, Buhuri, Madaba, Temeke, Vituo vya Mabuki na Kikulula. Kampasi ya Temeke haina huduma ya malazi hivyo, watakaojiunga itabidi wajitegemee. Pia katika Kampasi / Vituo vyetu wanachuo wa ufadhili binafsi watakaopenda kukaa nje ya chuo wanaruhusiwa.
3. Wakala inakaribisha maombi kutoka kwa vijana waliomaliza kidato cha Nne wanaotaka kujiunga na mafunzo ngazi ya Astashahada. Pia vijana waliomaliza Kidato cha Sita na wale wenye Astashahada katika fani zinazohusiana na kozi wanazoomba kwa ajili ya kujiunga na mafunzo ngazi ya Stashahada.
4. Kampasi zitakazohusika na mafunzo hayo ni kama inavyooneshwa kwenye jedwali hapa chini:

Na KAMPASI/ KITUO   ANUANI  KOZI ZITOLEWAZO
1. TENGERU S.L.P 3101 Arusha DAHP, SDDT & CAHP (Bweni na kutwa)
2. MPWAPWA  S.L.P 51 Mpwapwa DAHP & CAHP(Bweni na kutwa)
3. MOROGORO  S.L.P 603 Morogoro DAHP, DRMTC & CAHP (Bweni na kutwa)
4. BUHURI  S.L.P 1483 Tanga CAHP(Bweni na kutwa)
5. MADABA  S.L.P 568 Songea DAHP & CAHP(Bweni na kutwa)
6. TEMEKE S.L.P 39866 DSM CVLT & DVLT (Kutwa)
7. MABUKI S.L.P 352 Mwanza CAHP (Bweni na kutwa)
8. KIKULULA  S.L.P 147 Karagwe CAHP (Bweni)

5. Sifa za mwombaji
i) Stashahada (Diploma – DAHP, DRMTC, DCVLT) - Miaka miwili (2) kwa wanachuo waliomaliza kidato cha sita na mwaka mmoja (1) kwa wanachuo waliomaliza cheti kwa mfumo wa Semesta
Awe amemaliza elimu ya Kidato cha Sita kufaulu masomo matatu ya Sayansi kati ya Baiolojia, Kemia, Fizikia, Hisabati, Jiografia, Sayansi kimu na Kilimo. Kiwango cha chini cha ufaulu kitakachomwezesha muombaji kukubaliwa ni cha subsidiaries mbili kwenye masomo ya sayansi. AU

 • Awe amemaliza mafunzo ya Astashahada (Certificate) katika fani ya Animal Health and Production (AHPC), Agrovet au Certificate in Agriculture and Livestock Production (CALP) ambayo ni sawa na NTA Level 5 kwenye vyuo vilivyosajiliwa na NACTE.

ii) Astashahada (Certificate – CAHP, CVLT) – Miaka miwili (2)

 • Awe amemaliza Kidato cha Nne na kufaulu masomo matatu ya sayansi kati ya Baiolojia, Kemia, Fizikia, Hisabati, jiografia na Kilimo. Kiwango cha chini cha ufaulu kitakachomwezesha muombaji kukubaliwa ni cha alama ya D kwenye masomo matatu ya sayansi.

iii) Stashahada Maalum ya Teknolojia ya Maziwa (SDDT) – Miezi sita (6)

 • Mwombaji awe amefaulu katika ngazi ya Stashahada katika fani zifuatazo: Uzalishaji wa Mifugo (DAP), Afya ya Mifugo (DAH) na Afya na Uzalishaji wa Mifugo (DAHP).
 • Mwombaji awe amefaulu katika ngazi ya Shahada katika fani zifuatazo: Sayansi ya Wanyama, Afya ya Mifugo, Teknolojia na Usindikaji wa vyakula

6. Masharti ya Uombaji

 • Mwombaji atume fomu za maombi ya kozi anayotaka kusomea kwa kujaza fomu akiambatanisha nakala (photocopies) za vyeti vyake vya elimu, pamoja na cheti cha kuzaliwa.
 • Fomu inapatikana kwenye Kampasi zetu, vituo vyetu vyote na Tuvuti ya Wizara Website: www.mifugouvuvi.go.tz /organization /Agencies/LITA
 • Fomu irudishwe na Bank pay-in slip ya Tshs 20,000/= iliyolipwa kwenye LITA Revenue Account, NMB Morogoro, Acc. No. 22110003142
 • Fomu zote zitumwe Makao Makuu ya Wakala na siyo kwenye Kampasi za Mafunzo kwa kutumia anuani ya hapo chini.

7. Gharama za Mafunzo
Gharama za mafunzo zimeonyeshwa kwenye fomu ya maombi ambayo inapatikana kwenye Kampasi, vituo vya Wakala na tovuti ya Wizara Website: www.mifugouvuvi.go.tz /organization /Agencies/LITA
8. Mwisho wa kupokea maombi
Mwisho wa kupokea fomu za kujiunga na masomo ni tarehe 15/07/2015.
9. Taarifa kwa watakaochaguliwa
Majina ya watakaochaguliwa yatatangazwa kwenye magazeti ya Daily News na Habari Leo, kwenye mbao za matangazo za Wizara, Kampasi, Vituo vyake vyote na kwenye tovuti: www.mifugouvuvi.go.tz /organization /Agencies/LITA

10. Utaratibu wa kutuma fomu za maombi

Fomu za maombi zitumwe kwa:
KAIMU MTENDAJI MKUU,
WAKALA WA VYUO VYA MAFUNZO YA MIFUGO - LITA,
Veterinary Complex
131 Nelson Mandela Road
S. L. P 9152,
15487 DAR ES SALAAM

Please note that this information has expired.


Change for tangazo..

Please centre the table


Posted by mmaliwanga at 10 Jul 2015 14:59:34